Golikipa wa Real Madrid, Diego Lopez amekasirishwa na hali ya mabo ilivyo hivi sasa ndani ya klabu yake hiyo. Hali hiyo imekuja mara baada ya klabu hiyo kumfungukia nyanda huyo kwa kumwambia kuwa hana tena mafasi ndani ya Magalaktiko hao kutokana na timu hiyo kukamilisha dili la kumnyakua nyanda wa Lavente Keylor Navas.
Maamuzi na maneno hayo yanaonekana kumkasirisha sana Lopenzi ambaye wakati wakiwa kwenye ndege kutoka nchini marekani na magalaktiko hao walikwenda kushiriki michuano ya Champions cup aliwabwatukia miongoni mwa wakurugenzi wa ufundi waliokuwa kwenye ndege hiyo kwa kuwaambia " Mimi ni bora na mnalifahamu hilo ila mnachotaka kufanya dhidi yangu siwezi kuwazuia kwani ninyi ndio wenye maamuzi ya mwisho" huku akiwatazama nyusoni mwao.
Post a Comment