Mlinzi mbeligiji anaye kipiga kwenye klabu ya washika mitutu ya jiji la London (Arsenal) Thomas Vermaelen amefunguka hadharani hii leo na kudai kuwa kwa sasa mawazo na fikra zake ziko United na si mahala pengine popote pale.
Klabu ya Barcelona nayo inaisaka saini ya Mbeligiji huyo kwa udi na uvumba lakini thom mwenyewe amefunguka kwa kusema anapaona Old Trafford kuwa ndio makazi yake mapya siku chache zijazo.
Gaazeti la Daily Mail la kule nchini uingereza limesema kwamba Thomas ana mchumba Mwingereza ambaye pia ni mwana mitindo Polly Parsons,na mtoto wao mdogo wa kiume ambaye kamwe hatakua radhi kumuacha upweke nchini England na kutimukia mahali pengine pindi atakapotoka Arsenal.
Kauli hiyo inaonekana kuwa mwiba mchungu kwa klabu ya Barcelona ambayo nayo ina mihitaji mlinzi imara wa kati bara baada ya kustaafu kwa mlinzi na nahodha wake Carles Puyor.
Lakini pia yako mambo kadhaa ambayo ameyataja kuwa kivutio kwake kutua Man Utd nayo ni uhakika wa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza ambayo imekua hadithi pale Emirates akini pia uwepo wa rafiki yake mkubwa Robin van Persie ndani ya klabu ya Manchester United.

Meneja wa Manchester United Louis van Gaal anamtaka Vermaelen ili atimize malengo yake ya kuwa na mlinzi wa kati anayetumia mguu wa kushoto ikiwa ni muonekano mpya wa kikosi chake lakini pia wakati mwingine amtunie upande wa kushoto kwa Luke Shaw ambaye amebakia peke yake mara baada ya kuondoka kwa nahodha wa wamani wa United Mfaransa Patrice Evra aliyetimukia Juventus.
Post a Comment