Bosi wa Hull City, Steve Bruce anatarajia kuwa na usiku wa kukumbukwa hii leo ple ambapo kwa mara ya kwanza atakua akiiongoza klabu ya Hull Citty kuwavaa AC Trencin kwenye mchezo wa kufuzu kwaajili ya michuano ya Europa League pale kwenye dimba la KC Stadium.
"Natarajia utakua mmoja kati ya michezo mikubwa na wakukumbukwa, Tulikua na kitu kingine kikubwa pia nacho ni fainali ya kombe la FA ambapo ndipo ambapo klabu ilaanza safari hii ya hatua ambayo leo hii tumeifikia."
"Twendeni tukapambane na ninatarajia tutafuzu kwa ajili ya hatua ya makundi ambayo itakua ni historia nyingine tena katika historia ya soka barani ulaya.Hii itamaanisha jambo flani kwa mtu mmoja mmoja na klabu kwa ujumla endapo tutafanikiwa kwa hatua inayofuata"
Michuano hii ni moja kati ya michuano mikubwa barani Ulaya ambapo mabimwa wake huwa wanacheza mchezo dhidi ya mabingwa wa michuano ya UEFA Champions League.
Post a Comment