0

city_057 
 
 Manchester City imetangaza rasmi kuwa italipa mshahara wote wa mchezaji Frank Lampard anayekipiga kwa mkopo kutoka klabu ya  New York City   ya huko nchini marekani.
 
Mapema wiki hii mtandao huu ulichapisha habari iliyokua inamuhusu meneja wa timu ya Arsenal mfaransa Arsene Wenger akishangazwa na kulalama juu ya dalili za wazi zinazooneshwa na klabu ya Manchester City ya kuvunja sheria mpya ya manunuzi na matumizi ya UEFA inayojulikana kama  Financial Fair Play.
 
Frank Lampard amesajiliwa bure na klabu ya New York City ambayo wamiliki waki pia ni wamiliki wa klabu ya Manchester City. Klabu hiyo imeamua kumtoa Lampard kwa mkopo kwakua ligi ya huku nchini Marekani MLS inatarajiwa kuanza kuchanja mbuga kuanzia mwezi Machi mwakani.


Post a Comment

 
Top