Paul Gascoigne Gazza amelazwa tena hospitali kwa mara nyingine mara baada ya kuokwotwa na wana usalama akiwa chakari kutokana na kunywa pombe kupita kiasi.
Mkongwe huyu aliyeitumikia timu ya taifa ya Uingereza takribani michezo 57 alikutwa kwanye chumba chake cha kupanga cha ghalama nafuu huko kwenye mtaa wa Poole, Dorset, akiwa na mfuko wa plasiti ukiwa umejaa chupa kadhaa za pombe kali.
Taarifa zinasema kuwa Gazza alitimuliwa kwenye moja ya nyumba za kupanga katika mitaa hiyo kutokana kelele ziliyopitiliza, hivyo kuondolewa kinguvu kwenye nyumba hiyo aliyokua amepanga.
Post a Comment