0

as_drogba1
Klabu ya Chelsea inahofia kuwa huenda ikazikosa huduma za mshambuliaji mpya iliyemnasa kutokea klabu ya Garatasaray ya huko nchini Utoruki Didier Drogba kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu yanayomsibu.

Gazeti la the Mirror limeripoti kuwa Chelsea wanahofu kuwa maumivu aliyoyapata Drogba yanaweza kumuweka nje ya uwanja hadi miezi minne. 
 
Lakini bado klabu hiyo imeendelea kujipa moyo kuwa maumivu aliyoyapata mshambuliaji huyo yatakua yamekwisha ndani ya wiki kadhaa na sio miezi kama inavyofikiriwa.

Post a Comment

 
Top