Mabingwa wa Zambia Nkana wameendelea kuwapashia misuli moto klabu ya National Al Ahly ya nchini Misri mara baada ya hapo jana kukipiga kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa zamani wa Afrika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mabingwa hao wa kutoka nchini Zambia wamefungwa jumla ya magoli 2-0 kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Kamalondo mjini Lubumbashi.
Mpaka mapumziko Mazembe ilikua mbele kwa goli 1-0, goli lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Mali Ousmane Cisse wakati lile la pili likikwamishwa wavuni na na mchezaji wa zamani wa Chipolopolo Given Singuluma kabla ya mapumziko.
Nkana wanautumia mchezo huu wa kirafiki wa kujipima ubavu kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wao wa kundi B wa michuano ya Shirikisho barani Afrika (Confederation Cup) mchezo ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 9 ya mwezi huu pale mjini Kitwe nhini Zambia.
Mabingwa hao wa Zambia wako katika nafasi ya tatu katika kundi lao wakiwa na alama nne ikiwa ni alama nne nyuma ya vinara wa kundi hilo Al Ahly mar baada ya kila timu kucheza michezo takribani minne.
Halikadhalika Mazembe nao wako katika michuano ya klabu bingwa afrika (CAF Champions League) na wikiendi hii watakua mjini Lubumbashi ikiwakaribisha na kumenyana klabu ya Al Hilal ya Sudan kwenye mchezo wa kundi A.
Post a Comment