Kiungo raia wa chile anayekipiga ndani ya klabu ya vibibi vizee vya Turin (Juventus) Arturo Vidal amenaswa na mapaparazi akisaini jezi ya klabu ya Manchester United.
Mapaparazi hao wamemnasa Vidal ambae yuko ziarani na klabu yake ya Juventus huko nchini Australia ambako vibibi vizee hao wamejichimbia kwa minajili ya kufanya maandalizi ya mwanzo mpya wa msimu wa ligi kuu huko nchini Italia yaani Seria A.
Siku za hivi karibuni Vidal amekua akihusishwa sana kuhamia klabu ya Manchester United ambayo iko katika mipango madhubuti ya kukiimarishakikosi chake mara baada ya kutokuwa na msimu mzuri wa ligi kwa msimu uliokwisha.
Ziko taarifa zinazodai kwamba Vidal amekwisha kubaliana kila kitu na klabu ya Manchester United na kinachosubiriwa ni makubaliano tu baina ya vilabu viwili hivyo ili Vidal akaanze kuyatumikia majukumu yake mapya.
Post a Comment