0

 



Thomas Vermaelen amesaini mkataba wa miaka mitano na klabu ya Barcelona baada ya Wakatalunya hao kukubali kutoa kiasi cha paudi milioni 15 na kumnyakua mbeligiji huyo kutoka Arsenal.

Manchester United nayo ilikua ikihusishwa na kumsajili mchezaji huyo lakini mapema hii leo ilijitoa kwenye dili hilo mara baada ya kutakiwa kumtoa kwa klabu ya Arsenal mchezaji Chris Smalling kama sehemu ya mabadilishano.

Ni usajili wapili kwa nafasi ya ulinzi kwa klabu ya Barcelona mara baada ya miezi kadhaa iliyopita kutangaza usajili wa mlinzi wa klabu ya Valencia Mfaransa  Jeremy Mathieu  kwa ada ya paundi milioni 20.

Post a Comment

 
Top