Arsene Wenger rasmi amemtaja Mikel Arteta kuwa ndio nahodha mpya wa klabu ya Arsenal mara baada ya kuondoka kwa Thomas Vermaelen aliyejiunga na klabu ya Barcelona ya huko nchini Hispania.
Muhispania Arteta jana alikua chachu ndani ya kikosi cha Aresenal kilichofanikiwa kuwavurumisha mabingwa watetezi wa EPL klabu ya Manchester City kwa jumla ya magoli 3:0 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii uliofanyika jana kwenye uwanja wa Wembley.
Wenger pia amemtaja Mjerumani Per
Mertesacker kuwa ndiye atakayekuwa makamu nahodha wa washika bunduki hao wa jiji la London.
Arteta, mwenye umri wa miaka 32, anaingia kwenye msimu wake wa tatu na klabu ya Arsenal ana uzoefu wa kutosha na kazi ya unahodha kwani tayari amekwisha wahi kuwa nahodha wa kikosi cha Everton kilichokua kikiongozwa na meneja David Moyes.
Alipoulizwa na waandishi wa habari kuwa nani sasa anakwenda kuwa nahodha wa Arsenal mara baada ya kuondoka kwa Vermaelen Wenger alijibu "Mkuu ni Arteta na msaidizi ni Mertesacker".
Lakini pia alipoulizwa kuhusiana na pengo lililoachwa na nahodha wake wa zamani Wenger alisema anatarajiwa kumtumia Calum
Chambers kama mlinzi wa kati na mchezo dhidi ya Man City kilikua ni kipimo tosha cha kijana kuonesha uwezo na uhodari wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja pindi awapo uwanjani.
Wenger pia hakusita kuanika wazi mipango yake ya kutaka kuongeza wachezaji wawili ndani ya kikosi cha Arsenal na akasema miongoni mwa wachezaji hao pia anatarajia kumsajili mlinzi wa kati ili kijana Calum
Chambers atumike zaidi kama mlinzi wa pembeni.
Post a Comment