Manchester United wanamtazma kiungo veterani wa klabu ya Real Madrid Xabi Alonso kama ni tiba mbadala ya pengo la kiungo mkabaji ndani ya klabu hiyo.
Gazeti la The Daily Express la nhini Uingereza limeandika United wanataka kutuma ofa kwa klabu ya Real madrid yenye lengo la kutaka kupata saini ya kiungo huyo wa zamani wa klabu ya Liverpool.
Alonso ameibuka kuwa mmoja kati ya wachezaji walio kwenye mpango wa bosi wa klabu ya Manchester United Louis Van Gaal kufuatia kipigo walichokipata kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya nchini Uingereza dhidi ya Swansea lakini pia maumivu ya mara kwa mara yanayomkabili kiungo tegemezi wa timu hiyo Michael Carrick.

United kwa kiasi kikubwa inahusishwa na kutaka kuzinasa huduma za kiungo wa Chile anayekipiga Real Madrid Arturo Vidal kwenye majira haya ya joto lakini pia meneja Van Gaal amekua akihusishwa na kuwania saini ya kiungo wa AS Roma Kelvin Strootman.
Inaonekana dili la uhamisho wa Vidal ni kama vile liko mguu ndani mguu nje kutokana na msimamo wa mabosi wa klabu yake ya Juventus na pia Strootman anaonekana kukosa uzoefu wa kutosha kitu ambacho kinamfanya LVG kumuacha mchezaji huyo aendelee kukomaa ndani ya klabu yake kwa kipindi kingine zaidi na kuamua kumgeukia Alonso.

Post a Comment