Didier Drogba amrtangaza rasmi kuachana na soka la kimataifa. Hii inamaanisha kuwa sasa timu ya taifa ya Ivory Coast itakua ikiongozwa na nahodha mwingine kabisa na si Drogba kama ilivyozoeleka kwa miaka kadhaa.
Drogba mwenye umri wa miaka 36 amewatumikia Tembo wa Ivory Coast takribani michezo 104 na mara ya mwisho ikiwa kwenye fainali za kombe la Dunia kule nchini Brazil.
"Inahuzunisha sana kwani leo hii natangaza rasi kuachana na soka la kimataifa.Ninafuraha kuwa nahodha wa Ivory Coast kwa takribani miaka minane na nimelisaidia taifa langu kufikia anga za kimataifa na kushiriki michuano takribani minne ya kombe la Dunia na michuano mitatu ya mataifa ya Afrika."

"Sina maneno mazuri sana ninayoweza kuwaeleza mashabiki na wakaelewa haswa kwa upendo na sapoti yao katika kipindi chote hiki. magoli yangu yote, zawadi zangu zote na kila aina ya ushindi tuliokua tukiupata nautoa kwao kama kumbukumbu yao kwangu na ya kwangu kwao.
"Lkini pia shukrani zangu ziende kwa wachezaji wenzangu tuliokua tukishirikiana vyema nyakati zote, waalimu wangu tangu wa awali mpaka mwalimu wangu wa sasa Herve Renard kwa kuonesha upendo mkubwa kwangu. niwatakie kila la kheri na umoja ndani ya timu yetu.I."
Post a Comment