Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Real
Madrid Christiano Ronaldo amemshauri mchezaji mwenza wa Real Madrid Angel di
Maria kuachana na nia ya kutaka kujiunga na klabu ya Manchester United.
Bosi wa klabu ya Manchester United
Ed Woodward alikuwepo mjini Cardiff usiku wa jana akiwashuhudia Real wakishinda
fainali ya European Super Cup akiwa na nia ya kufungua mazungumzo na Di Maria.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa moja ya
gaazeti maarufu la El Confidencial wanasema Ronaldo anaamini kuwa Di
Maria ni mmoja kati ya wachezaji muhimu ndani ya Los Blancos achilia mbali
kuwasili kwa James Rodriguez na anataka mpango huo ufanyike wakati mwingine na
si sasa.
Mabosi wa Real Madrid wanataka
kumuuza Di Maria kwakuwa thamani yake iko juu kwa sasa lakini Meneja Carlo
Ancelotti bado anazihitaji huduma za Muargentina huyo.
Taarifa zinadai kuwa Mashetani
Wekundu wameweka mezani kiasi cha paundi milioni 55 kwaajili ya Di Maria lakini
kauli ya Ronaldo inaweza kuwa chachu katika kulicheleweshsa dili hilo.
Post a Comment