Louis van Gaal amewaagiza mabosiwa klabu yake ya Manchester United kuhakikisha wanaharakisha dili la kumleta haraka Angel di Maria ndani ya Old Trafford.
Gaazeti la The Sunday Mirror la huko nchini Uingereza limeandika kuwa LVG amemuagiza Makamu mwenyekiti wa vigogo hao
Ed Woodward kuhakikisha anapambana kwa ajili ya kuinasa saini ya mshambuliaji huyo.
"Tunahitaji kuwa na mshambuliajiwa pembeni wa kiwango cha juu duniani anayefanana na Ronaldo au Bale,Ukitazama wachezaji hao wote wawili wana mikataba ya muda mrefu na Real, mtu pekee ambaye anafanana na watu hao kwa sasa duniani ni Di Maria ambaye mkataba wake unaelekea ukingoni na anaomekana kama hana nafasi tena ndani ya Real Madrid.
Katika kuonesha kuwa ni kwakiasi gani anamuhitaji mshambuliaji huyo LVG aliamua kulitaja jina la Di Maria na akimuweka katita daraja moja na washabuliaji Gareth Bale na Chiristiano Ronaldo hali inayoonesha ni kama vile kumshinikiza makamu mwenyekiti Ed Woodward kuharakisha dili hilo.
Mapema wiki hii klabu ya Paris Saint-Germain yakule nchini Ufaransa ilijitoa rasmi kwenye mbio za kumsajili Di Maria kwa madai kuwa kitita cha pesa cha paundi milioni 50 kinachotakiwa na Real Madrid ni kikubwa mno ukilinganisha na thamani halisi ya mshambuliaji huyo.
Luis van Gaal anaaminikuwa kikosi cha klabu ya Manchester United alichokirithi kutoka kwa mtangulizi wake David Moyes hakijatengemaa na alipoul8zwa uwezekano wa Woodward kuvunja rekodi ya dunia alisema huo ndio mpango waklabu ya Manchester united kufanya hivyo kwa sasa.
"Kwa sasa tuna namba 9 watano na namba 10 wanne katika kikosi chetu na hatuna winga anayeweza kusukuma mashambulizi mbele.Kwa kifupi ninachoweza kusema kuwa hatuna winga anayefanana na Ronaldo au Di Maria katika kikosi chetu, hivyo inatulazimu kucheza kwa mtindo tofauti kidogo na ule tunaotaka na kutarajia kuucheza kucheza"
Post a Comment