1. Alexis Sanchez - Arsenal
Huu ni usajili mkubwa wa pili kwenye rekodi za usajili za klabu ya Arsenal ambapo amemghalimu kiasi cha paundi milioni 32 Mfarasansa Arsene Wenger ambapo amemsajili mshambulizi huyu wa
Chile kwenye viwanja vya Emirates kutoka klabu ya Barcelona.
Akitarajiwa kuwa mchezaji wa akiba pale Camp Nou mara baada ya kuwasili kwa Luis Suarez, Alexis aliamua kuikataa ofa ya Liverpool na kuamua kujiunga na Arsenal.
Ni mchezaji anayetegemewa sana kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Chile ambaye mashabiki wengi wa Arsenal wanatarajia mengi na makubwa kutoka kwake haswa la kumaliza ukame wa vikombe ndani ya klabu ya Arsenal tangu mwaka 2004.
2. Diego Costa - Chelsea
Baada ya kupachika takribani mabao 36 katika mashindano yote aliyoshiriki akiwa na klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid na kuisaidia klabu hiyo kunyakua ubingwa wa ligi ya Hispania na kucheza fainali ya UEFA Champions League hatimaye Mhispania huyu mwenye asili ya Brazil ameamua kujiunga na klabu ya Chelsea kwa ada ya paundi milioni 30.
Jose Mourinho mara kadhaa msimu uliopita alikua akiikosoa safu yake ya ushambuliaji kuwa ilikua ikiundwa na baadhi ya wachezaji ambao ni wazee lakini pia akiwataja kuwa sio wa kiwango cha Dunia, hali iliyopelekea Chelsea kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Mourinho sasa anatumaini jipya kutoka kwa Costa kwani anaamini kuwa kutokana na uwezo wake wa kupachika mabao atakwenda kukata kiu ya ufungaji aliyokua ikikosekana klabuni hapo kwenye msimu wa 2013-14.
3. Cesc Fabregas - Chelsea
Huyu ni mtu mwingine tena ambaye Mourinho anamtarajia kuipeleka Chelsea kwenye kilele cha mafanikio. Nahodha huyo wa zamani wa klabu ya
Arsenal ametua Stamford Bridge kwa ada inayotajwa kuwa nia paundi milioni 27.
Baada ya kutumia miaka mitatu akiwa na Barcelona mara baada ya kujiunga nayo kwa mara ya pili akitokea klabu ya Arsenal mnamo mwaka 2011 Fabregas, mwenye umri wa miaka 27,anatarajiwa kuleta athali kubwa kwenye klabu ya Chelsea.
Mourinho anamtaja Fabregas kama ndiye mrithi mpya wa Frank Lampard aliyetimuka klabuni hapo mara baada ya mkataba wake kuisha na kujiunga na klabu ya New York City kabla ya kuamua kujiunga kwa mkopo wa miezi sita kwenye klabu ya Manchester City.
Ushirikiano wake na Diego Costa unatarajiwa kuipaisha Chelsea na hatimaye kuipatia ubingwa wa EPL.
4. Adam Lallana - Liverpool
Kiungo mwenye utulivu na ufundi mwingi, Lallana ndiye aliyekua dereva wa mashambulizi wa klabu ya Southampton kwenye Premier League msimu uliopita.
uwezo wake binafsi ulimfanya apate nafasi kwenye kikosi cha timu ta taifa ya Uingereza kwenye michuano ya Kombe la Dunia kule nchini Brazil lakini pia uhamisho wa mamilioni ya pesa kwenda kwenye klabu ya Liverpool ambapo ataungana na viungo bora wengine kama akina
Philippe Coutinho na Raheem wakati ambapo klabu hiyo ya pale Merseyside itakua ikijaribu kufanya vyema zaidi ya msimu wa 2013-14.
5. Romelu Lukaku - Everton
Lukaku ndio aliyekua uti wa mgongo wa sehemu ya ufungaji kwa klabu ya Everton kwenye msimu uliopita ambapo ameifungia jumla ya magoli 15 kwenye Premier
League akiitumikia timu hiyo kwa mkopo kutoka klabu ya Chelsea na kumsaidia Meneja Roberto Martinez kumaliza katika nafasi ya tano kwenye msimu wake wa kwanza tangu atue pale kwenye viwanja vya Goodison Park.
Martinez amevutiwa sana na uwezo wa Mbelgiji huyu na hivyo kuwashawishi mabosi wa Everton kumleta pale Merseyside moja kwa moja kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 28.
Kufuzu kwaajili ya michuano ya Uefa Champions League ndio shabaha kuu kwa klabu ya Everton kwa msimu huu na Lukaku ndiye anayebebeshwa jukumu hilo hasa kitengo cha upachikaji mabao.
6. Eliaquim Mangala - Manchester City
Manchester City wameshinda kikombe cha Premier League msimu uliopita lakini wanaonekana wakiwa na mapungufu haswa sehemu ya ulinzi ya timu hiyo.
Hii ndio sababu Meneja Manuel Pellegrini ameamua kutoa kitita cha paundi milioni 42.9 kumjumuisha Mfaransa Mangala pale Etihad
Stadium kutoka klabua ya Fc Porto.
Ushirikiano wake na nahodha Vincent Kompany utakwenda kufanya sehemu ya ulinzi ya klabu ya Manchester City kuimarika zaidi.
7. Dejan Lovren - Liverpool
Brendan Rodgers akiwaongoza Liverpool walifanikiwa kufunga jumla ya magoli 101 lakini 13 pungufu ya Manchester City ambao waliutumia mwanya huo na kuwa mabingwa wapya kwa tofauti ya alama 2.
Rodgers amekua akimtafuta mrithi wa kiungo wa ukabaji mara baada ya kujiuzulu kwa Jamie Carragher, na Lovren, inaaminika kuwa ndiye mtu mujarabu kwa nafasi hii.
Amenunuliwa kwa ada ya paundi milioni 20m kutoka Southampton, na anatarajiwa kuja kuimarisha sehemu ya kiungo ya Liverpool hasa kiungo cha ukabaji.
8. Ander Herrera - Manchester United
United ikiwa inaongozwa na David Moyes, ilijaribu kumshawishi Herrera kujiunga na mashetani wekundu hao siku ya mwisho ya usajili msimu uliopita.
Uhamisho huu ulishindikana lakini miezi 12 baadae United wamefanikiwa kumpata Herrera kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 30 kutoka klabu ya Athletic Bilbao.
Kiungo halisi wa Kihispania anavyocheza, Ufundi uwezo wa kupiga pasi kumemfanya Herrera kumshawishi meneja wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal kumuona kama ni mmoja wa suluhisho la sehemu ya kiungo endapo atashirikiana vyema na Michael Carrick pindi atakapo rejea kutika kwenye majeraha yanayomsibu.
9. Luke Shaw - Manchester United.
Mgeni mwingine kwenye kikosi cha Luis Van Gaal kwaajili ya kuleta mapinduzi ndani ya Old Trafford, United
imemfanya Shaw kuwa ndiye kinda ghali zaidi duniani kwa kulipa ada ya uhamisho wa paundi milioni 30 kutoka klabua ya Southampton.
Kama ilivyo kwa Lallana na Lovren nae alikua ni mmoja kati ya uti wa mgongo wa klabu ya Southampton ambayo ilikua na mafanikio kwenye msimu uliopita.
Luis Van Gaal anatarajia kumtumia Shaw kama ndio mrithi atakayeziba ombwe lililoachwa na mkongwe Patrice Evra.
10. Bojan Krkic - Stoke City
Wakati fulani alidhaniwa kuwa ndiye mrithi wa Lionel Messi baada ya kupandishwa kutoka klabu ya vijana wa Barcelona lakini Bojan amepoteza dira na muelekeo katika miaka ya hivi karibuni.
Ameshatolewa kwa mkopo kwenye vilabu vya AC Milan, AS Roma na Ajax lakini kote ameshindwa kupata nafasi ya kuendelea kusalia kwani amekua akipita kama majira ya mwaka yanayokuja na kuondoka.
Post a Comment