Klabu ya Manchester United inaonekana kuwa tayari kuwajumuisha washambuliaji Danny Walbeck na Javier Hernandez (Chicharito) ili kuharakisha kulifanikisha dili la kumnasa kiungo mahiri raia wa Chile anayekipiga kwenye klabu ya Juventus Arturo Vidal.
Gazeti la The Daily Star limeripoti kuwa United wamewapa Juve ofa ya paundi milioni 32 na kuchagua mmoja kati ya wachezaji hao wawili ili kukamilisha dili hilo la kumnasa kiungo huyo mchezeshaji.
Swali la msingi linalobakia vichwani mwa wadadisi wa mauala ya kisoka ni kuwa ni nani kati ya wanandinga hawa wawili atakayetolewa kama sadaka kwenda Juventus na pia klabu ya Juventus nayo itavutiwa na nani baina ya Chicharito na Danny Welbeck ili kumnasa Vidal
Ikumbukwe tayari meneja wa klabu ya Manchester United Louis Van Gaal alikwisha mwambia Welbeck kuwa milango iko wazi kwake kuondoka ndani ya Manchester United na kwenda kwenye klabu yoyote ambayo itaonesha nia ya kumuhitaji.
Post a Comment