Kiungo wa zamani na mwenye ufundi mwingi wa klabu ya Mancester United paul Scholes anatarajiwa kurejea tena uwanjani. Scholes anatarajiwa kurejea uwanjani siku ya August 11 kwenye mchezo wa ngao ya hisani unaotarajiwa kuwahusisha wachezaji kadhaa wa zamani wa vilabu vya Manchester United na Bayern Munich.
Paul Scholes, Bryan Robson na Edwin van der Sar ni miongoni mwa wacheaji wa zamani wa Uniteda wanaotarajia kuwepo kwenyea mchezo huo dhidi ya Munich ukiwa na lengo la kuchangia jamii (watoto) unaotarajia kufanyika kwenye dimba la Allianz Arena.
Paul Breitner aliyekua nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani Magharibi kwenye fainali za kombe la Dunia mwaka 1974 ndiye atakayekua nahodha wa kikosi cha Munich ambacho kitamjumuisha pia mchezaji wa zamani wa vilabu vyote viwili Owen Hargreaves na Mholanzi Marc van Bommel.
Kikosi cha United kitawajumuisha pia Dwight Yorke, Andy Cole na Ronny Johnsen ambao walikuwemo kwenye kikosi cha United kilichoifanyia maajabu ya kukumbukwa Bayern kwenye fainali ya UEFA Champions League mwaka 1999 pale mjini Barcelona kwenye dimba la Nou Camp. Pesa zitakazo patikana zitakwenda kwenye mfuko ujulikanao kama Allianz Foundation kwaajili ya kuwasaidia watoto.
Post a Comment