0

Montsho wa Botswana anatumia dawa haramu
Bingwa wa zamani wa dunia wa mbio za mita 400 Amantle Montsho kutoka Botswana amepigwa marufuku ya kushiriki mashindano ya fainali ya mbio za mita 400 baada ya vipimo vya chembe chembe ya damu yake kutambua kuwa alikuwa ametumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.
Uchunguzi wa kwanza ulitambua kuwepo kwa dawa aina ya methylhexaneamine ambayo imepigwa marufuku.

Vipimo vya pili vimepelekwa mjini London uingereza kwa uchunguzi zaidi na pia kudhibitisha kuwepo kwa mabaki ya dawa hiyo inayooongoza nguvu mwilini.Vipimo hivyo vilichukuliwa punde baada ya bingwa huyo wa zamani wa Jumuiya ya madola kumaliza katika nafasi ya nne katika mchujo wa kufuzu kwa fainali za mita 400.

Montsho, 31, ndiye bingwa mtetezi wa nishani ya dhahabu ya jumuiya ya madola.
Aidha aliwahi pia kushinda nishani ya dhahabu ya dunia katika mwaka wa 2011.
Tineja kutoka Nigeria aliyepokonywa nishani ya dhahabu kwa kutumia madawa yaliyopigwa marufuku.
Montsho ambaye alishindwa na muingereza Christine Ohuruogu katika mashindano ya Moscow alikuwa ameiambia BBC kuwa anapania kustaafu punde baada ya kushiriki mashindano ya Olimpiki yakayokuwa huko Rio de Jenairo mwaka wa 2016.
Kulingana na utafiti wa shirikisho la kupambana na madawa ya kuongeza nguvu mwilini WADA
Montsho, 31 ndiye mwanariadha wa pili kutoka Afrika kupatikana kuwa alitumia madawa hayo haramu.
Mwanariadha wa Nigeria Chika Amalaha wa alipokonywa nishani yake ya dhahabu majuzi na akahukumiwa marufuku

Post a Comment

 
Top