0
as_chicharito

Klabu ya Juventus ya huko nchini Italy imetuma ofa kwa klabu ya Manchester United kwa minajili ya kumnasa mshambuliaji Javier Hernandez (Chicharito). 

Kwa mujibu wa gazeti la Tuttosport lahuko nchini Italy limethibitisha kwamba Juve wameweka mezani ofa ya paundi milion 4.75 ili kunasa saini ya Mmexico huyo anayeonekana kuto kuwa na amani ndani ya United tangu ujio wa meneja mpya Luis van Gaal.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Manchester United zimesema kwama kwa sasa Chicharito anafikiria zaidi mustakabali wake nje ya united kwani imethibitika kuwa hayuko tayali hata kukaa na Van gaal kwa minajili ya kujadili mustakabali wake ndani ya United.

Chanzo hicho pia kimethibitisha kuwa katika kuonesha ni jinsi gani Juve wanamuhitaji Chicharito wamesema wako tayari kukaa meza moja na United kujadili kumchukua mchezaji huyo kwa mkataba wa mkopo wa muda mrefu.

Post a Comment

 
Top