KLABU ya Tottenham imekamilisha usajili wa Pauni Milioni 4 wa mchezaji wa Sporting Lisbon, Eric Dier.
Klabu hiyo ya Kaskazini mwa London imezipiga bao Newcastle na West Ham na kumtia ping ya miaka mitano Muingereza huyo katika jitihada za Mauricio Pochettino kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ulinzi ambayo msimu uliopita iliruhsu mabao 51.
Dier, akizungumza na tovuti ya Tottenham, amesema amefurahi kuhamia White Hart Lane msimu ujao: "Nimevutiwa haswa kujiunga na klabu kubwa kama hii katika Ligi Kuu England,".
Post a Comment