Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni na aliyezoea vya kunyonga kamwe vya kuchinja haviwezi. Misemo hiyo ya wahenga imejidhihirisha hii leo ambapo mchezaji wa zamani wa Napoli na timu ya taifa ya Argentina Diego Maradona ameyazua majanga mengine tena.
kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Argentina aliyejawa na vingi vituko kwenye maisha yake ya ndani na njee ya uwanja safari hii amemnasa kibao mwandishi wa habari aliyekua akimfuatilia kutaka kumuhoji alipokua akitoka kwenye chumba cha upasuajia katika moja ya hospitali huko nchini Argentina.
Kwa mujibu wa gaazeti la El
Comercio, la huko nchini Argentina limeandika kuwa Maradona alikingia kwenye mabishano na majibizano na mwandishi huyo aliyekua akimfuatilia kitendo ambacho hakikumfurahisha Maradona.
Maradona alisikika akisema “Hii ni zawadi kwa mtoto wangu. Hii ni siku yangu ya kwanza nikiitumia nikiwa na mwanangu. Ninafuraha sasa kuachana na masuala ya mpira wa miguu, kwa kuwa nina umri wa miaka 53 kwa sasa na pia mimi sio “Dieguito”, jina langu ni Diego Armando Maradona!”
Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona, Napoli na Boca Juniors alitoka ndani ya gari yake na kumfokea mwandishi huyo huku akimtazama usoni kwa kumkazia macho.
“Wewe ni mjinga? unacheza na maisha yangu wakati mimi sichezi na yakwako?”alimuuliza mwandishi huyo kabla ya kumchapa kibao na kuondoka.
Maradona mara kadhaa amekua akiingia kwenye matatizo na jamii, vyama vya soka na waandishi wa habari ikumbukwe tayari alishawahi kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili na miezi kumi kwa kuwajeruhi waandishi wanne kwa kuwashuti kwa bunduki kubwa ya kujifunzia shabaha.
Post a Comment