Samuel Eto'O huenda likawa ni moja kati ya jina la kustaabisha na kushangaza kwenye orodha ya usajili wa wanandinga wapya ndani ya klabu ya Liverpool msimu huu.Magaazeti mengi ya huko nchini Uingereza leo hii yameipa uzito wa juu na kufanya uchambuzi wa kina juu ya kile ambacho Eto'o anaweza kukileta na kukichangia ndani ya Liverpool.
Mchezaji huyu wa kimataifa wa Cameroon yuko huru hivi sasa mara baada ya kuondoka ndani ya klabu ya Chelsea kutokana na mkataba wake kumalizika na tayari wawakilishi wake wamekutana na mabosi wa Liverpoo ili kukamilisha uhamisho huo.
Brendan Rodgers anapambana kujalibu kutatua tatizo la mshambuliaji wa mwisho ndani ya kikosi cha Liverpool na anamtazama Eto'o kama ni mmoja kati ya suluhisho la tatizo linalomkabili kwa sasa.Vilabu vya Ajax, West Ham na QPR vimeonekana kuvutiwa na Eto'o.
Eto'o's amekua akihitaji mshahara mkubwa sana jambo ambalo lilitokea kuwa tatizo kwa klabu ya West Ham, lakini Liverpool hili kamwe haliwezi kuwa tatizo kutokana na ukweli kwamba Liverpool ni moja kati ya klabu ambayo imejijenga sana kiuchumi.
Post a Comment