Manchester Unitd rasmi imingia mazungumzoni na klabu ya Real Madrid yenye lengo la kuwanyakua Angel di Maria na Sami Khedira kutoka kwa Magalaktiko hao.
Jana Meneja wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti alithibitisha taarifa zilizokua zimzagaa jijini Madrid kuwa wachzaji wawili hao wamegoma kuongeza mkataba na mabingwa hao wa Ulaya na hivyo kuthibitisha kuwa wachezaji hao wawili wanaweza kuondoka kwenye majira haya ya kiangazi kabla ya dirisha la usajiri kufungwa.
Gazti la The Manchester Evening News limandika kuwa Meneja wa timu hiyo Louis van Gaal anatarajiwa kujaribu bahati yake kwa kujaribu kuwasajiri Khedira na Di Maria kwa wakati mmoja kutoka Madrid.
Wadadisi wa mambo wanadai kuwa klabu ya Real Madrid wako tayari kuikubali ofa yoyote itakayokua inazidi paundi milioni 20 kwaajili ya Sami Khedira.
Lakini pia ikumbukwe kuwa makamu mwenyekiti wa klabu ya Manchester United Ed Woodward tayari alikwishaanza kufanya mazungumzo na mabosi wenzake wa Real Madrid yenye lengo ya kukamilisha dili la paundi milioni 50 kwaajili ya kumnasa Di Maria.
Endapo usajiri huu utakamilika unaweza kurejesha furaha kwa mashabiki wa Manchester United ambao wanaonekana kukasirishwa na mwenndo mbaya wa usajili wa klabu hiyo.
Taarifa njema kwa mashabiki wa klabu hiyo ni kurejea mazoezini kwa mshambuliaji wake tegemezi Robin van Persie akijiandaa kwaajili ya mchezo wa Barclays Premier League dhidi ya Sunderland siku ya jumaapili.
Post a Comment