Mabingwa wa Ujerumani klabu ya Bayern Munich wanaonekana kuwa mstari wa mbele katika kuiwania saini ya kiungo Sami Khedira kutoka klabu ya Real Madrid.
Habari zinasema kuwa Bavarian wanaonekana kuwa mstari wa mbele katika kuiwania saini ya kiungo huyo hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kuwazidi kete vilabu vya Arsenal, Manchester United na Chelsea ambao wanaonekana kupigana vikumbo kuwania saini ya mchezaji huyu wa kimataifa wa Ujerumani.
Madrid wanajiandaa kumuuza Khedira mara baada ya kumnunua Toni Kroos na James Rodriguez kwenye majira haya ya kiangazi na inaaminika kuwa Bayern wako tayari kumpatia mkataba wa muda mrefu mchezaji huyo.
Sami Khedira yuko na klabu ya Real madrid tangu mwaka 2010 alipojiunga akitokea klabu ya VfB Stuttgart lakini amekua akipambana na maumivu ya mara kwa mara tangu kuwasili kwake ndani ya Les Blancos.

Post a Comment