Liverpool imefikia makubaliano na klabu ya AC Milan ya manunuzi ya Mario Barotelli kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 16.
Barotelli aliyekua akifanya mazoezi kwenye uwanja wa mazoezi wa AC Milan Milanello training complex alikatisha mazoezi na kuondoka akiwa kwenye gari yake ya rangi nyekundu aina ya Ferrari aliwaambia waamndishi wa habari waliofurika uwanjani hapo kuwa hakuna cha kuficha sasa kwani leo ndio siku yake ya mwisho kuwepo nchini Italy na anakwenda kujiunga na vijogoo hivyo vya Anfield.
Kwa minajili hiyo basi ni jukumu la Meneja Brendan Rodgers kumjumuisha au kutomjumuisha mshambuliaji huyu kwenye mchezo wa jumatatu dhidi ya timu yake ya zamani ya Manchester City.
Balotelli mchezaji aliye na vituko vingi ndani na nje ya uwanja amekua akihusika katika matukio kadhaa ya kustaajabisha baina ya watu wa kada mbali mbali wakiwemo wachezaji na mameneja wake katika vilabu anavyovichezea.
Ndani ya uwanja moja kati ya matukio yanayosalia vichwani mwa watu ni kitendo cha kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo baina ya klabu yake ya zamani ya Manchester City dhidi ya Arsenal mnamo mwaka 2012 kwenye mchezo ambao uliwaondoa Man City kwenye mbio za ubingwa.
Lakini pia ataendelea kukumbukwa kwa kauli yake aliyoiandika kwenye flana yake ya ndani kwenye mchezo ambao waliwafanyia udhalilishaji wapinzani wao wa jadi wa mji mmoja Manchester United alipoibuka na maandishi yaliyokua yakisomeka 'Why Always
Me?' ikiwa ni majibu kutokana na tukio la kumtimua mfanyakazi wa kikosi cha kudhibiti moto nyumbani kwake.
Kubwa kuliko ni pale walipokunjana na Meneja wake wa wakati huo Roberto Mancini mara baada ya kutokea hali ya sintofahamu baina yake na Mjerumani Jerome Boateng hali iliyopelekea kutimuliwa kwenye uwanja huo wa mazoezi.
Akiwa na umri wa miaka 24 tu Super Mario akiwa akatika ligi ya nchi mbili tofauti amekwishashinda mataji manne ya ligi kuu moja la ligi ya mabingwa, moja la chama cha soka cha uingereza yaani FA Cup na moja la Coppa Italia.
Post a Comment