Rafael da Silva, Marouane Fellaini, Luis Nani, Oliviera Anderson, Wilfried Zaha,Will Keane na Javier Hernandez wameambiwa na Meneja wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal kuwa wanaweza kuondoka klabuni hapo kwakuwa hawako ndani ya mipango ijayo ya Manchester United.
Van Gaal jana amekutana na mchezaji mmoja mmoja binafsi kwa malengo ya kuzungumza nao na amewaarifu wachezaji Fellaini, Zaha, Nani na Keane kwamba klabu itakuwa tayari kusikiliza ofa kutoka kwa klabu yoyote ile itakayokuwa inawahitaji.
Rafael, ni moja kati ya majina ambayo yamewaacha midomo wazi wadadisi wengi wa masuala ya soka kwani hakuna aliyetarajia kuwa angeweza kuoneshwa mlango wa kutokea na Van Gaal.Inasemekana kuwa LvG anataka kumtafuta mlinzi wa pembeni mwingine ambaye ndiye atakua mbadala wa Rafael.
Kagawa mmoja kati ya wachezaji ambao walikua wakitajwa sana kuwa wataoneshwa mlango wa kutokea ndani ya United amenusurika kwenye kadhia hiyo kwani sasa atakua msaidizi wa Wahispania Ander Herrera na Juan Mata kwenye sehemu ya kiungo cha ushambulizi.
Kiungo Olivieira Anderson na mshambuliaji Javier Hernandez wote walikua wakifahamu kuwa United ilikuwa iko tayari kusikiliza ofa kutoka kwa vilabu vya Southampton, Inter Milan, Tottenham, Atletico Madrid na
Juventus ambavyo vilionesha kumuhitaji Chicharito wakati Napoli inamuhitaji
Fellaini ambaye inasemekana kuwa United ndio wanaouchelewesha mchongo huo kukamilika.
Newcastle imeonesha kumuhitaji sana Wilfred Zaha, sambamba na vilabu vya Crystal Palace, West Ham na Nottingham Forest.
Post a Comment