Kocha wa timu ya taifa ta Uingereza Roy Hodgson amewapa ushauri wa bure wachezaji wa kiingereza kutoka na kuenda kucheza nje ya Uingereza ili kupata uzoefu utakaowasaidia kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa.
Hodgson ameuambia mtandao wa FA.com kuwa zaidi ya nusu ya wachezaji aliowateua kuunda kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kilichoshiriki michuano ya kombe la Dunia nchini Brazil mwaka huu walikua hawana uhakika wa namba za kudumu kwenye vikosi vya kwanza vya vilabu vyao wanavyovichezea kwenye ligi kuu ya Uingereza.
"Napendelea kuwaona wachezaji wa Kiingereza wakijumuishwa kwenye vilabu bora vya nje ya Uingereza kulikoni kukaa katika benchi hapa Uingereza."
"Lazima tukubaliane na ukweli kwamba endapo wachezaji wetu watatoka na kwenda kucheza nje ya nchi watapata uzoefu mkubwa ambao utatusaidia pindi watakapopata nafasi ya kujumuishwa kwenye kikosi cha timu yetu ya Taifa watakua na nafasi nzuriya kuutumia uzoefu walioupata huko ili kuleta ushindi kwa taifa letu.
'Sio kazi yangu kuwaambia au kuwashauri wachezaji nini cha kufanya kuhusiana na maisaha yao ya soka bali ni mtazamo na maoni yangu kama mwalimu anayetamani kuona anapata mchanganyiko wa wachezaji watakaomletea ushindi kwenye michezo yake." Alimalizia kusema Roy Hodgson ambaye kikosi chake cha timu ya taifa cha Uingereza kitakua kinajitupa kwenye uwanja wa Wembley siku ya tarehe 28 Septemba kumenyana na Norway.
WACHEZAJI WA KIINGEREZA NJE YA NCHI |
---|
Ashley Cole - Roma (Italy) |
Luke Steele (Golikipa)- Panathinaikos (Ugiriki) |
Matt Jones (Golikipa) - Belenenses (Ureno) |
Kenny Pavey - AIK Stockholm (Sweden) |
Jordan Stewart - San Jose Earthquakes (Marekani) |
Bradley Wright-Phillips - New York Red Bulls (Marekani) |
Charlie I'Anson - Alcoron (Hispania) |
Post a Comment