0



Klabu ya Chelsea imemtoa kwa mkopo wa muda mrefu kiungo Oriol Romeu kwa klbu ya VfB Stuttgart kwa mkopo wa msimu mzima.

Romeu amekua akitumika sana na mkufunzi Jose Mourinho kwenye michezo ya kabla ya msimu wa ligi huko nchini Marekani.

Kiungo huyo Muhispania mwenye umri wa miaka 22 ameichezea Chelsea takriban michezo 33 tu tangu alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2011 akitokea klabu ya Barcelona ya nchini Hispania; na msimu uliokwisha aliumalizia akiwa na kikosi cha Valencia kinachoshiriki La Liga  ya huko kwao Uhispania.

Hivi majuzi Oriol Romeu alisaini mkataba wa miaka mitatu ya kuendelea kuitumikia klabu Chelsea hali iliyompa matumaini ya kuwemo kwenye mipango ya mkufunzi Jose Mourinho.

Post a Comment

 
Top