0
as_reus
Barcelona inapambana kuwasainisha viungo wa Borussia Dortmund na Fiorentina Marco Reus na Juan Cuadrado kabla ya kuanza kutumikia adhabu yao ya kufungiwa kufanya usajili waliyopewa na FIFA.

Barca wataanza kutumikia adhabu ya kutokusajili January 16 baada ya rufani yao waliyoikata kuhusiana na adhabu hiyo kukataliwa hapo jana na shirikisho hilo na hivyo kutakiwa kuanza kuitumikia adhabu hiyo kama kawaida pindi muda utakapofika.

Baada ya adhabu hiyo kukataliwa Barcelona sasa imepanga kuwasajili wachezaji hao mapema iwezekanavyo na mara baada ya usajili huo kukamilika wachezaji hao watatolewa kwa mkopo kwenye vilabu vyao ambako watavitumikia vilabu vyao kwa msimu mzima wa ligi unaofuata.

Barca wamefikia maamuzi hayo ili kuinusuru klabu hiyo na adhabu inayokwenda kuitumikia kuanzia Januari 16 ambapo itawalazimu kukaa misimu miwili bila ya kufanya usajili wakiwa katika kutumikia adhabu waliyopewa na FIFA mara baada ya kukiuka taratibu za usajili za shirilisho hilo la kabumbu Duniani

Post a Comment

 
Top