Klabu ya Arenal inahofu ya kumkosa dimbani mshambuliaji wake Mfaransa Olivier Giroud kwa takribani miezi mitatu kutokana na kuwa na tatizo la mguu alilolipata kwenye mchezo dhidi ya Everton siku ya jumaamosi.
Giroud aliyeiokoa timu yake isiambulie kichapo kwa kuisawazishia magoli yote mawili akitokea benchini anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya mara ya pili ili kutanabahisha ukubwa wa tatizo lake.
Hata hivyo taarifa za kitabibu zimesema kuwa wanachotaka kukifanya klabu ya Arsenal ni kujiridhisha tu kwani tayari taarifa rasmi zinadai kuwa mchezaji huyo anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki mbili licha ya hofu iliyotanda kwa sasa kuwa huenda mchezaji huyo akaugulia maumivu kwa miezi takribani mitatu.
Meneja wa klabu ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger sasa anaonekana kulazimishwa kufufua tena mahitaji yake kwa Mfaransa mwenzake Loic Remy ambaye alionesha dalili za kutaka kumjumuisha kwenye kikosi cha washika bunduki hao.
Lakini pia endapo uchunguzi huo wa mara ya pili utathibitisha kuwa Giroud sasa atakwenda kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu basi jambo jingine analoweza kulifanya Mfaransa huyu ni kuhakikisaha dili la uhamisho wapaundi milioni 10 wa mshambuliaji Lukas
Podolski halikamiliki kwa sasa.
Podolski aliomba kuondoka ndani ya klabu ya Arsenal kutokana na kukosa uhakika kwenye kikosi cha kwanza kitu ambacho alipewa maraka zote ma mzee Wenger kwa sharti moja tu kuwa timu itakayomtaka ni lazima wafikie ada ya uhamisho ya paundi milioni 10.
Tayari vilabu vya
Juventus, Wolfsburg na Galatasary, vilionesha nia ya kutaka kumnasa mshambuliaji huyo lakini kuumia kwa Giroud kunamaanisha huenda Mfaransa huyo akaweka ngumu kukamilika kwa dili hilo.
Arsene Wenger anatarajiwa kutoa taarifa kamili leo hii kwenye mazungumzo na waandishi wa habari kabla ya mchezo wa kesho wa kuwania kufuzu kwa michuano ya UEFA Champions League siku ya jumaatano dhidi ya Besiktas ya Uturuki.
Maumivu ya Giroud sio tu kitu pekee ambacho kinampa kiwewe Mfaransa huyo bali kukosekana kwa Aaron Ramsey aliyepewa kadi nyekundu kwenye mchezo wake wa mwanzo dhidi ya Besiktas na Mikel Arteta anayeugulia maumivu ta enka ni jambo jingine linalompa wakati mgumu mzee Wenger.
Post a Comment