0
Early silverware: Arsenal beat Manchester City 3-0 to win the Community Shield at Wembley on Sunday Baada ya miaka takribani tisa ya kuwa na ukame wa makombe klabuni hapo Arsenal leo hii imeongeza ndoo nyingine kwenye kabati lake mara baada ya kuwavurumisha bila huruma klabu ya Manchester City kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii uliofanyika kwenye uwanja wa Wembley.

 
Arsenal imeonekana kuwapa raha mashabiki wake hii leo kwani licha ya kandanda safi na la uhakika  walilolitandaza lakini pia ni upana wa kikosi chao kwani licha ya mauaji hayo ya kimbali waliyowafanyia Man City bado wachezaji wake kadhaa wakutumainiwa hawakuhusika kwenye mchezo huo akiwemo kiungo Mjerumani mwenye ufundi mwingi Ozil.

Mockery: Arsenal fans poked fun at the City supporters by doing the 'Poznan' celebration after the third goal 
Arsenal leo hii imewakosa wachezaji wake watatu wa kutumainiwa ambao ni Mesut Ozil, Per Mertesacker na Lukas Podolski ambapo meneja Mfaransa Arsene Wenger aliamua kumtumia Yaya Sanogo (Chanongo) ambye baadae alibadilishana na Giroud.

 
 
Swali jipya lililopo vichwani mwa mashabiki wengi wa soka na kuhusiana na hali ya mahusiano baina ya meneja wa Man City na golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Uingereza Joe Hart ambye alikuwepo tu benchini kwenye mchezo wa leo.
 
 Having a gaze: Caballero flung himself at the strike but ended up being nowhere near it
 
Willy Caballero ndiye aliyesimama kwene lango la Manchester City hii leo na Gael Clichy alitumika kama mlinzi wa kulia wakati Micah Richards alikuwa amekaa tu kwenye benchi la Man City na maamuzi ya wakuwatumia wachezaji chipukizi Dedryck Boyata na Matija Nastasic kama walinzi wa kati.
 
 Try getting this back! Yaya Toure holds off the challenge of Wilshere with consummate ease 
Ushindi huu unamaanisha jambo kwa klabu ya Arsenal japo ni mapema sana kuwataja kama mabingwa wapya wa msimu huu kwani hata msimu uliokwisha Manchester United ndio walikua mabingwa wa Ngao ya Jamii lakini wakamaliza Ligi wakiwa katika nafasi ya saba.

Watching brief: The respective managers - Wenger (left) and Manuel Pellegrini - stand on the touchline

Post a Comment

 
Top