Bodi ya ligi kuu nchini Uingereza imeagiza spray 2,000 kama zilizokua zinatumika kwenye kombe la dunia kuwekea alama. Wiki iliyopita FA iliuthibitishia umma kuwa waamuzi wa ligi kuu nchini Uingereza kwa msimu huu watatumia spray hiyo kama ilivyokua kwenye michuano ya kombe la Dunia kule nchini Brazil.
Spray hizi pia zinatarajiwa kutumika kwenye michezo ya Champions League na Europa League kwa msimu huu wa 2014-2015.Kwa mara ya mwanzo kabisa Spray hii itaonekana ikitumika kwenye mchezo wa Ligi kuu wakati ambapo
Manchester United watakapowakaribisha Swansea City hapo August 16 kwenye dimba la Old Trafford.
Bodi hiyo ya ligi imetangaza kuwa maamuzi hayo ya kuitumia Spray hiyo yamekuja mara baada ya watu wengi kushauri kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa ni moja kati ya vitu vizuri vilivyowahi kutokea katika tasnia ya mpira wa miguu ambapo bodi hiyo ya ligi inatakiwa itumie ili kuepusha baadhi ya matatizo yanayoweza kujitokeza uwanjani.
Post a Comment