0
Good workout: Scholes was captaining a United XI in a charity game vs Bayern Munich at the Allianz
Katika kile kinachoonekana kama kuonesha thamani na heshima kubwa kwa kiungo huyo anayeaminika kuwa ni moja kati ya viungo bora kwa kizazi cha sasa kiungo wa Bayern Munichen na timu ya taifa ya Ujerumani Bastian Schweinsteiger ameomba jezi ya kiungo Paul Sholes hapo jana.

Kiungo huyo aliyekuwepo kwenye uwanja wa Allianz Arena akishuhudia mchezo wa hisani baina ya wachezaji wa zamani wa klabu za Manchester United na Bayern Munich alishuka kwenye ngazi haraka wakati wa mapumziko kwenda kumuomba Scholes jezi yake jambo ambalo lilikubaliwa na Sholes ambaye baadae aliwaambia waandishi wa habari kuwa hiyo ni heshima kubwa kwake.

 Big fan: Schweinsteiger made a swift move to nab the legendary midfielder's shirt at the break

 "Nimempa jezi yangu Schweinsteiger ambayae alikuja kuniomba wakati wa mapumziko lakini na yeye alinipatia ya kwake amabyo inaonekana nzuri kwani inatoka kwa mmoja kati ya viongo bora kabisa duniani kwa sasa, Ametoka kushinda kombe la Dunia siku chache zilizopita na kuzungumza tu na mtu wa kalba yake ni jambo la faraja pia."


Interview: Scholes told a reporter after the game about where his original shirt from the game had gone


"Ni jambo zuri na la faraja sana kubadilishana jezi na mchezaji aliyetoka kushinda kombe la Dunia lakini pia aliyeshinda vikombe kadhaa na klabu yake ya Bayern Munich.Scholes alifunga goli la pili kati ya matatu ya timu yake ya wakongwe wa Manchester united kwenye mchezo ambao uliishia kwa sare ya magoli 3-3.

Post a Comment

 
Top