Meneja wa klabu ya Southampton Ronald Koeman anasubiri
jibu kutoka kwa mabosi wa klabu ya Manchester United kuhusiana na dili la mauzo
ya mshambuliaji wa Mashetani wekundu hao Javier Hernandez ( Chicharito)
Meneja Koeman anataka kumnyakua Mmexico huyo
na kumleta ndani ya is St Mary's, lakini tatizo linabakia kwa mchezaji mwenyewe
ambaye anaonekana kufanya machaguo ya wapi aelekee mara baada ya kuoneshwa
mlango wa kutokea na meneja Luis van Gaal.
Klabu ya Southampton imetoa masaa 48 wawe
wamepatiwa jibu la mwisho na mshambuliaji huyo kabla hawajachukua maamuzi ya
kumtafuta mshambuliaji mwingine.Manchester United wanataka kitita cha paundi
milioni 9.5 kwa klabu itakayokua tayari kutoa kiashi hicho kikiwa kamili au
paundi milioni million 11.5 kwa klabu itakayokua tayari kulipa kwa awamu mbili
kwa zaidi ya miezi 12.
Post a Comment