Kocha mpya wa klabu ya Barcelona Luis Enrique amemwambia kiungo Mkameroon anayekipiga katika timu hiyo Alex Song kwamba hayuko katika mipango yake ya msimu huu hivyo anaweza kutimuka na kuelekea akutakako.
Kwa mujibu wa gaazeti la El mundo de Portivo la huko nchini Spain limeandika kwamba kocha Enrique amekutana na Song na Ibrahim Afellay na kuwaambia kuwa wawili hao wawamo kwenye mipango yake ya mbio za ubingwa wa mashindano mbalimbali msimu huu.
Kiungo huyo wa zamani wa klabu ya Arsenal amezungumzia uwezekano wa kurejea tena kwenye EPL na amekua akihusishwa sana na klabu za Liverpoo na Manchester United.
"Ikiwa nitaondoka Hispania nitarejea kwenye Premier League, Nitarejea nchini Uingereza siku moja nakuhakikishia." Alisema Song alipokua akifanya mahojiano na moja kati ya vituo vya Televisheni nchini Cameroon.
Post a Comment