Mshambuliaji raia wa Ujerumani aneyekipiga kwenye klabu ya arsenal Lukas Podolski amewatibua mashabiki wa klabu hiyo ikwa ni masaa kadha tu mara baada ya timu yao ya washika mitutu wa jiji la London Arsenal kupoteza kwa jumla ya magoli 2:1 dhidi ya klabu ya Swansea hapo jana.
Wengi wa mashabiki hao wakionekana wakiwa na huzuni kubwa kutokana na matokeo hayo, Lakini Podolski aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake maalumu wa tweeter akizungumzia kuanguka kwa ukuta uliokuwa ukiigawanya nchi yake ya Ujerumani katika vipande viwili vya Ujerumani Mashariki na Magharibi pale alipoandika; " Ni miaka 25 sasa imepita tangu ukuta uliokuwa unaigawanya ujurumani mpaka mwaka 1989 ulipovunjwa lakini sasa tuko wamoja"
Wakati yeye akisherehekea maadhimisho hayo ya miaka 25 baadhi ya mashabiki wa klabu ya Arsenal wameonekana kukerwa na kitendo hicho hali iliyopelekea kumjibu na kumshauri kujiheshimu kidogo kwani kwa mtazamo wao wanaona kuwa haiwezekani wao wafungwe halafu yeye aandike ujumbe wa namna hiyo kwenye mtanadao huo wa kijamii.
Post a Comment