0
Wojciech Szczesny admits Arsenal were outdone by moments of brilliance from Chelsea on the dayMlinda mlango namba moja wa klabu ya Arsenal Wojciech Szczesny amedai kuwa tatizo linaloikabili timu yake hiyo ni kukosa nidhamu ya mchezo,dira na muelekeo wa mashindano. Maneno hayo mazito aliyatoa masaa kadhaa baada ya timu yake hiyo kushuhudiwa ikipoteza kwa jumla ya goli 2:1 dhidi ya Swansea wakati wao ndio waliokua wa mwanzo kuanza kuliona lango la Swansea.

Szczesny amesisitiza kuwa kwa sasa the Gunners ni lazima iimarishe sehemu yake ya ulinzi ambayo mara kadhaa imetokea kuwaghalimu katika mashindano mbalimbali ambayo klabu hiyo inashiriki.

"Sehemu kubwa ya mchezo tulionekana kuimarika katika kila idara kwenye mchezo dhidi ya Swansea, tulikua na ukuta imara lakini pia sehemu ya ushambuliaji tulionekana kuwa na njaa ya kusaka ushindi, lakini tulikua na dakika tano mbaya sana mwishoni mwa mchezo zilizotufanya tupate matokeo tofauti kabisa na matarajio na matakwa yetu kwa ujumla."

"Ni kitu ambacho tunatakiwa kukifanyia kazi sisi sote kwa ujumla wetu kwani tayari kimekwisha tokea kwenye michezo miwili na vinaonekana kutugharimu kwenye mashindano na harakati zetu za mbio za ubingwa."

Post a Comment

 
Top