0
Keane clashes with Patrick Vieira during a game at Highbury, a common sight in the Premier LeagueArsenal ina takribani wiki moja kusahau maumivu iliyoyapata mnamo dakika 20 za michezo miwili muhimu iliyoicheza. Hapa nazungumzia mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya Underletch na ule wa ligi kuu ya Uingereza uliomalizika kwa klabu hiyo kupoteza kwa jumla ya magoli 2:1 dhidi ya Swansea City a.k.a Swanselona. 

The Gunners ilimkosa kiongozi ndani ya uwanja ambaye angeweza kuwaongoza na kuwahimiza wenzake kwa kadri muda ulivyokua ukiyoyoma, lakini timu haikuunganishwa vyema katika idara mbalimbali, kiungo kilikua kikicheza kimpango wake halikadhalika kwa sehemu ya ulinzi na ushambuliaji.

Arsenal's current midfield lacks the steel and prowess of players like Patrick Vieira (left) and Emmanuel Petit
Waliokabidiwa majukumu ya kuiunganisha timu katika idara zote tatu walishindwa kabisa kuyatekeleza majukumu yao kwani hakukuwa na mshikamano kabisa dimbani.

Suluhisho pekee analoweza kulifanya Mfaransa Arsene Wenger  kuinusuru klabu hii kwa sasa ni kuhakukusha kuwa Arsenal inamsainisha mchezaji ambye atakuja kuwa kiongozi ndani ya timu hiyo, kiuhalisia wachezaji wa kalba hii kwa sasa duniani wamekwisha toweka na kama wapo basi ni wachache sana.

 Alan Shearer celebrates scoring one of his 260 Premier League goals... his record still stands
Hapa nawazungumzia watu kama akina Patrick Viera a.k.a Injini ya Meli, Roy Keane,Frank Lampard,Tonny Adams, Alan Shearer na wengi wengineo. 

Na hata hapa hapa kwetu kibongobongo nawazungumzia watu ambao kwa miaka ya karibuni tu wameonesha uwezo wa kuwaongoza wenzao dimbani Suleymani Matola a.k.a Veron Salvatory Edward 'Doctor' Juma Kaseja, Saidi Mwamba Kizota, John Kabisama yule wa Majimaji FC ni mfano mmoja wapo wa wachezaji wa kalba hii wanaohitajika sana ndani ya kikosi cha klabu ya Arsenal.

Wafuatao ni wachezaji ambao mimi kwa mtazamo wangu ninaona wanasifa ya uongozi na wanaweza kuwa watu muafaka sana kwa klabu hii kulitatua tatizo hili linalowakabili.

1) Mats Hummels

 Three leaders Arsenal could sign to add a spine to gutless Gunners
Mats Hummels ameripotiwa kuwa na nia ya kutaka kutua Arsenal mnamo mwezi January na nikitu ambacho kwangu mimi nakiona ni sahihi mno.

Mlinzi huyu aliyeiongoza vyema timu yake ya taifa la Ujerumani kutwaa taji la kombe la Dunia kule nchini Brazil ndiye nahodha wa klabu ya Dortmund ambaye anauzoefu wa kutosha katika majukumu yake ya kiuchezaji na yakiuongozi.

Kiasili Hummels mwenye umri wa miaka 25 ni kiongozi  na amejitahidi kupambana kuwa mmoja kati ya wachezaji wa hadhi ya juu duniani lakini tatizo ninaloliona kama ni kikwazo kwenye usajiri wake ni ada ya uhamisho ya paundi milioni 30 wanazozitaka Dortmund ili waweze kumruhusu kuondoka klabuni hapo.

Wasiwasi unakuja kutokana na tabia ya mzee Wenger na The Gunners kwaujumla ya kutopenda sana kuwanunua wachezaji kwa gharama kubwa hivyo huenda wakashindwa kukamilisha dili hili sababu kubwa ikiwa ni ada ya uhamisho inayotakiwa.

Siku za hivi karibuni tumemshuhudia mlinzi raia wa Brazil David Luiz akijiunga na klabu ya Paris Saint Germain kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 50 lakini ukiangalia kwa uwezo wa uwanjani bado mchezaji huyu kwa mtazamo wangu hamfikii Hummels.

2) Sami Khedira

 The German World Cup winner has rejected two offers of a new deal to stay at the Bernabeu
Sami Khedira anaweza kupatikana kiulaini kabisa mnamo mwezi wa January kutokana na hali ya mambo inavyoendelea sasa ndani ya klabu yake ya Real Madrid. 

Taarifa zinadai kuwa huenda ada ya uhamisho ya mchezaji huyu ikwa kama paundi milioni 8 tu kwani kwa sasa jamaa yuko kwenye kipindi cha mwishomwisho cha mkataba wake na magalactico hao.

Njia pekee wanayoweza kuifanya Arsenal ni kuwatega Real angalau kwa kampunga kanono kidogo japo hali ya Khedira kuwa na desturi ya kuumia umia inafanya kuwa na shaka kwa upande mwingine.

Huyu ni aina ya mchezaji ambaye ni sahihi kabisa kujumuishwa kwenye kikosi cha washika mitutu kwani ukiachilia mbali uimara wake na nidhamu yake mimi ninamuona mchezaji huyu kama ni mmoja wapo ya aina ya wachezaji wanaofiti kwenye mfumo wa kiuchezaji wa klabu ya Arsenal.

3) Luiz Gustavo

 On his way: Luiz Gustavo (right)  played for Brazil earlier this week before joining Wolfsburg
Huyu ni mchezaji ambaye mzee Wenger amekua akimhitaji kwa kipindi kirefu sasa na ninathubutu kusema ni uzembe wa mzee Wenger ndio uliomfanya mchezaji huyu kutoshika mitutu pale Emirates.

Huyu ni msaada mkubwa sana kwenye kiungo cha ukabaji, lakini kimo chake kinaweza kikawa msaada sana kwenye suala zima la mipira ya vichwa inayoweza kuwa hatari sana langoni mwa klabu ya Arsenal.

Tayari ushiriki wake kwenye michuano ya Champions League na World Cup unamfanya kuwa na kitu cha ziada anachoweza kuwapa Arsenal lakini yote kwa yote ni mmoja kati ya wachezaji wanaotamani kuudhihirishia ulimwengu kuwa the Bavarians walichemka kuamua kumuondoa kwenye kikosi chao.

Maono yangu yananituma kuwa endapo wawili kati ya watatu hawa watatua ndani ya washika mitutu hawa wa jiji la London basi mimi nadhani kuwa Arsenal itakua ni moja kati ya timu ngumu kabisa kufungika.

Naomba kuwasilisha.....................
                                                                                    hossamulaya.blogsport.com
                                                hossamulaya@gmail.com 
                                                   0755231571/0713281932.

Post a Comment

 
Top