Kijana mmoja aliyevamia uwanja ameudhihilishia umma ni jinsi gani anamkubali na kuvihusudu vitu vya mshambuliaji bora wa Dunia Cristiano
Ronaldo mara baada ya kuvamia uwanja na kukataa kumuacha Ronaldo aliyekuwa amemkumbatia kwa nguvu kama mtoto anayeomba hifadhi kutoka kwa mlezi wake kuhofia jambo fulani.
Kijana huyo aliluka kizuizi kilichowekwa kwenye dimba la Estadio de Los Carmenes mara baada ya kipyenga cha mwisho cha mwamuzi kilichokua kikiashiria kuwa Los Blancos wameibuka na ushindi wa jumla ya magolo 4:0 Mreno huyo akiwa wa mwanzo kabisa kufungua njia ya kuzifumania nyavu.
Mara baada ya kupata nafasi ya kumshikilia kwa nguvu mchezaji huyo na kutakiwa na walizni waliokuwepo eneo la tukio kumuachia kijana huyo aligoma na kuendelea kumshikilia kwa nguvu Ronaldo aliyeonekana kuwa mtulivu wakati tukio zima likichukua nafasi.
Post a Comment