Manchester United imefikia makubaliano ya paundi milioni 56 yenye lengo la kumnyakua mshambuliaji Radamel Falcao kwa mkataba wa kudumu mara baada ya mkataba wake wa mkopo wa muda mrefu utakapokwisha mwishoni mwa msimu huu.
United tayari wamekwisha fanya makubaliano binafsi na pande zote mbili yaani Monaco na Falcao na hivyo mara tu baada ya kukamilika mkataba wake wa mkopo wa muda mrefu wenye thamani ya paundi milioni 8 basi wanaweza kumnyakua mshambuliaji huyo.
Mabingwa hao mara 20 wa ligi kuu nchini Uingereza watakua na chaguo sasa kumpa mkataba wa kudumu mchezaji huyo endapo tu wataridhishwa na kiwango kilichooneshwa na mchezaji huyo lakini pia uzima wa mshambuliaji huyo aliyetoka kwenye maumivu.
Falcao
ambaye kwa sasa anajinyakulia kitita cha paundi 305,000 kwa wiki anatarajiwa kubakia na kiwango hicho hicho cha mshahara endapo tu dili hilo litakamilika.
Jambo la kutia faraja ni kuwa wakala wa Radamel Falcao anayetambulika kwa uhodari wake wa kazi hiyo Jorge Mendes, ana mahusiano ya karibu sana na klabu ya Manchester United lakini pia mchezaji mwenyewe ameonesha nia yake ya kutaka kubakia ndani ya Manchester United zaidi ya msimu ujao.
Licha ya dhana mbaya iliyojengeka juu ya uhamisho wa dakika za mwisho wa Radamel Falcao lakini United wamekua wakifanya makubaliano kadha wa kadha na wakala George Mendes kwa wiki kadhaa sasa kuhakikisha kuwa wanakamilisha dili la kumbakiza moja kwa moja mshambuliaji uyo wa timu ya taifa ya Colombia.
Makubaliano hayo ya mkataba wa muda mrefu yanawafanya United kumwangalia kwa ukaribu mchezaji huyo kutokana na ukweli kwamba mchezaji huyo ametoka kwenye maumivu makali ya kifundo cha mguu ambayo yalimfanya akae nje ya uwanja kwa takribani nusu yote ya msimu uliopita na kuzikosa fainali za kombe la Dunia.
Post a Comment