0
Loan ranger: Wellington Silva, who Arsenal signed from Fluminense, has joined Levante until the end of the season

Mshambuliaji mpya wa kibrazil wa klabu ya Arsenal Wellington Silva hatimaye sasa ataweza kuitumikia klabu yake hiyo kuanzia msimu ujao mara baada ya kupata kibali cha kufanyia kazi nchini Uingereza.

The Gunners ilimsainisha Silva, ambaye anatajwa kuwa Neymar mpya kutoka klabu ya Figueirense mnamo mwaka 2009 kwa ada inayokadiliwa kufikia paundi milioni 3.5 lkini hakuweza kuwatumikia washika bunduki hao kutokana na matatizo ya Visa hivyo kumfanya avitumikie kwa mkopo vilabu vya Alcoyano, Ponferradina, Real Murcia na sasa Almeria ya huko Uhispania.

Wellington sasa atakua huru kuitumikia Arsenal kuanzia msimu ujao mara baada ya kupewa uraia wa Hispania na hivyo kuwa huru kuingia nchini Uingereza.

 welly silva

Post a Comment

 
Top