0
Radamel Falcao usiku wa jana alifungua upya akaunti yake ya magoli kwenye karia ya kimataifa mara baada ya kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwaka mmoja kupita kwa kuiongoza timu yake ya taifa ya Colombia kuifunga El Salvador jumla ya magoli 3-0 jijini New York.

Radamel Falcao celebrates his first Manchester United goal against Everton at Old Trafford on Sunday

Falcao hajapata nafasi ya kujumuishwa kwenye kikosi cha mwalimu Jose Pekerman tangu November 19 mwaka jana wakati alipoichezea Colombia kwenye mchezo usio na magoli dhidi ya timu ya taifa ya Uholanzi baada la kuumia mfupa wa mguu wakati akiichezea timu yake ya Monacokombe la chama cha soka cha nchini Ufaransa (Coupe de France) mnamo mwezi January.

 Falcao (second left on his United debut against QPR) says he is feeling more comfortable back on the pitch

Maumivu hayo yalimlazimisha Falcao kujiondoa kwenye kikosi cha Colombia kilichokwenda kushiriki kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil na hivyo siku ya jana kurejea kivingine kabisa kwa kuifungia goli la kuongoza timu yake ya Colombia.

Falcao’s Monaco departure prompted protests from fans and United's new striker says he understands why

Falcao aliyevalia beji ya unahodha hapo jana ilimchukua dakika saba tu kwenye dimba la Red Bull Arena - mjini New York goli ambalo limemfanya Falcao kuwa mfungaji namba mbili wa muda wote wa timu ya taifa ya Colombia kwa kuwa na magoli 21 katika michezo 52 aliyoichezea timu hiyo.


Falcao aliifungia klabu yake ya Manchester United wiki iliyopita goli ambalo lilikua la kwanza pia kwa Mkolombia tangu ajiunge kwa mkopo na klabu hiyo akitokea klabu ya Monaco ya Ufaransa. 

Wadadisi wa masuala ya soka wanaamini kuwa kitendo cha Falcao kuzifumania nyavu katika michezo hiyo miwili itamuongezea kitu cha ziada mshambuliaji huyo kwani kutamfanya aongeze kujiamini na hivyo kurejea katika makali yake ya kawaida ya ufungaji wa mabao na hivyo wpenzi wa soka kuaza kuyaona tena makali ya The Tiger.

Post a Comment

 
Top