Ni jambo la kustaajabisha miongoni mwa wadadisi wengi wa masuala ya kisoka mara baada ya hapo jana shirikisho la soka ulimwenguni FIFA kutangaza majina ya wachezaji 23 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Dunia huku jina la Mruguay Luis Suarez likiwa halipo. Akiwa mmoja kati ya wachezaji waliofunga magoli 33 katika michezo 39 kwenye mashindano yote ya msimu uliopita na pia akitajwa kama mmoja wa wachezaji watukutu sana wasioweza kuzizuia hasira zao pindi wawapo uwanjani.
Anang'ata watu, kitendo ambacho amekifanya mara tatu katika mashindano na nchi mbalimbali, na ni juzi tu amerejea kutoka kifungoni ikiwa ni mara ya tatu kufungiwa kutokana na kosa hilo. Watu wengi sana wameshitushwa na kutokuwepo kwa jina la Suarez kwenye orodha hiyo ya FIFA, lakini kanuni ya 3 ya sheria za Ballon d'Or inaeleza wazi kwanini hauwezi kulijumuisha jina la Suarez na mtu mwingine yoyote yule mwenye tabia kama za kwake katika kinyang'anyiro hicho.
"Zawadi itatolewa kutokana na uwezo binafsi wa mchezaji uwanjani na tabia yake kwa ujumla akiwa ndani na nje ya uwanja" hivyo ndivyo kanuni hii inavyo sema.
Yafuatayo ni baadhi ya matukio aliyowahi kuyafanya mshambuliaji huyu na hivyo kumfanya kutokuwa na vigezo vya kujumuishwa kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo licha ya kuwa na uwezo mkubwa sana awapo dimbani.
June 2014 - Alimng'ata Giorgio Chiellini wa Italy kwenye mchezo wa raundi ya pili ya kombe la Dunia na kuambulia kifungo cha miezi minne.
April 2013 - Alimng'ata Branislav Ivanovic wa Chelsea kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza na kuambuliwa kifungo cha michezo 10.
Dec. 2011 - "Aliwaonesha kidole kinachoashiria matusi mashabiki wa Fulham na hatimaye kuambulia kifungo cha mchezo mmoja.
Dec. 2011 -Alikutwa na hatia ya kumtolea maneno ya kibaguzi aliyekuwa mlinzi wa klabu ya Manchester United Patrice na kupewa adhabu ya kufungiwa michezo 8.
Nov. 2010 - Alimng'ata Otman Bakkal alipokua akiichezea Ajax na kuambulia adhabu ya kufungiwa michezo 7.
July 2010 -Alioneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Ghana mara baada ya kuudaka kwa makusudi mpira uliokuwa unaingia wavuni.
Hivyo kutokana na matukio hayo hapo juu tena yakiwa ni baadhi tu ndio maana jina la mshambuliaji huyu halijajitokeza miongoni mwa wachezaji 23 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Dunia.
Post a Comment