0
Man United ready to finally sign Sneijder FOR FREE in January

Manchester United inajiandaa kumnyakua bure kiungo Mholanzi anayekipiga ndani ya klabu ya Galatasaray Wesley Sneijder kutokana na mchezaji huyo kutarajiwa kuwa mchezaji huru kuanzia mwezi January mwakani mara baada ya klabu ya Galatasaray kushindwa kumlipa mchezaji huyo kwa takribani miezi mitatu mfululizo. 

Sneijder amekua akiwindwa na na mabosi wa United kwa takribani miaka miwili iliyopita na mara kadhaa United wameshindwa kufikia ada ya uhamisho iliyokuwa ikitakiwa na vilabu vya Inter Milan na klabu yake ya sasa.

Hivyo basi meneja Louis van Gaal sasa anaweza kumnyakua kiungo huyo bure kabisa mnamo mwezi January mara baada ya kiungo huyo kuthibitisha kuwa itakapofika mwezi huo wa January atakua ametimiza miezi mitatu mfululizo bila kulipwa na hivyo kuufanya mkataba wake kuvunjika na hivyo kuweza kujiunga na klabu yoyote pasi na timu hiyo kuhitajika kulipa ada yoyote ile.


Post a Comment

 
Top