Manchester United msimu huu imejaribu kujiimarisha katika idara ya ushambuliaji kwa kufanya usajili wa kuvunja rekodi nchini Uingereza wakiwa na nia ya kutaka kurejesha makali yao yaliyopotea msimu uliopita lakini uwepo wa majeruhi takribani tisa ndani ya kikosi cha mashetani wekundu hao kinaifanya klabu hiyo kuweweseka.
Hivi karibuni klabu hiyo imetokea kumuamini mlinzi kinda
Paddy McNair aliyekuwa akishirikiana vyema na Muajentina Marcos Rojo katika kuimalisha ulinzi wa katikati wa klabu hiyo lakini katika kile kinachoonekana kama kuandamwa na jinamizi la mkosi wa majeruhi kijana huyu naye amelipotiwa kupata maumivu ya misuli daraja la tatu aliyoyapata siku ya Jumapili wakati timu yake ya Manchester United ilipokipiga dhidi ya Everton na kupata ushindi wa magoli 2:1.
Kuumia kwa McNair kunatimiza idadi ya walinzi watano wa wa klabu ya Manchester United wanaokaa nje ya uwanja kutokana na majeruhi ambapo wengine ni Luke
Shaw (kifundo cha mguu), Jonny Evans (kifundo cha mguu), Phil Jones (misuli) na Chris
Smalling (nyama za paja).
Wachezaji Ander
Herrera (mbavu), Jesse Lingard (kifundo cha mguu), Michael Carrick
(mguu) na Ashley Young (nyonga) nao wanaungana na walinzi hao watano katika orodha ya majeruhi ndani ya United wakati Wayne Rooney anaendelea kutumikia adhabu yake ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo dhidi ya West Ham.
Wakati Manchester United ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya majeruhi, Arsenal wao wanashika nafasi ya pili katika orodha hiyo na kibaya zaidi ni kuwa idadi kubwa ya wachezaji walio majeruhi kwenye kikosi cha Mfaransa Wenger ni wale wa kikosi cha kwanza.
Mikel Arteta, Aaron Ramsey,
Mathieu Debuchy, Olivier Giroud na Theo Walcott ni miongoni mwa wachezaji majeruhi wa klabu ya Arsenal na wengi wao ni wachezaji wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Ifuatayo ni orodha ta majeruhi katika vilabu mbali mbali vya EPL mpaka hivi leo:
ORODHA YA WACHEZAJI MAJERUHI KWA VILABU VYA PREMIER LEAGUE KWA MSIMU WA 2014/2015.
Manchester United -9
Arsenal- 7
Burnley -7
Everton -7
Newcastle -7
West Ham -7
Liverpool- 6
Southampton- 5
Chelsea -4
Stoke City- 4
Swansea City- 4
Aston Villa- 3
Hull City -3
Sunderland- 3
West Brom -3
Crystal Palace- 2
Leicester City- 2
Manchester City -2
Queens Park Rangers- 2
Tottenham Hotspur -2
Post a Comment