0
Monaco offer Wenger huge £28m contract to leave Arsenal
Klabu ya Monaco imeripotiwa kumpa mkataba mnono Meneja wa klabu ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger, mkataba unaokadiriwa kufikia kiasi cha paundi milioni 28 nia ikiwa ni kumshawishi Mfaransa huyo aachana na klabu yake ya Arsenal. 

Wenger ambaye tayari alikwisha wahi kuwa Meneja wa klabu ya Monaco kabla ya kuwa bosi wa washikamitutu hao wa jiji la London atatakiwa kutoa maamuzi ambayo anadhania yatakua sahihi na ya busara kwake katika kuutanabahisha mustakabari wake wa maisha yake ya kuongoza soka.

Inaaminika kuwa klabu ya Monaco imemuahidi Wenger mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya paundi milioni 9.3 kwa mwaka ambao utamfanya ajikusanyie kitita cha paundi milioni 28 katika kipindi chote cha miaka mitatu ya kandarasi yake hiyo anayotaka kupewa.

Inasemekana kuwa Wenger hajatoa jibu lolote lile mpaka sasa lakini siku zote amekua akisisitiza kuwa kamwe hawezi kuvunja mkataba na Arsenal ili aweze kujiunga na klabu nyinginezo yoyote ile.

Post a Comment

 
Top