Mara baada ya kulazimisha sare kwenye mchezo uliopita nimejaribu kukaa chini na kutazama baadhi ya mambo ambayo mimi nadhani mzee Wenger akiyafanya anaweza kutupa raha mashabiki wa Arsenal kuelekea mchezo wa UEFA dhidi ya Wabelgiji wa Anderlecht.
1) Calum Chambers achukue nafasi ya Nacho Monreal
Monreal amecheza kama mlinzi wa kati wakati Chambers alipokua anatumikia adhabu ya kadi huku Koscielny akiwa anajiuguza majeraha yakehivyo natamani kumuona kijana Chambers akirejea pahala pake ili kuimarisha ulinzi.
2) Mikel Arteta badala ya Mathieu Flamini
Flamini amekua kama homa za vipindi yaani sometimes yes sometime no kwa msimu huu lakini Arteta anakipaji kikubwa sana cha kucheza kiungo kwa upande wangu mimi. Mara baada ya kuwa fiti kwa asilimia miamoja nadhani ni wakati wake sasa kujumuishwa kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal ili kutupa radha.
Flamini amekua kama homa za vipindi yaani sometimes yes sometime no kwa msimu huu lakini Arteta anakipaji kikubwa sana cha kucheza kiungo kwa upande wangu mimi. Mara baada ya kuwa fiti kwa asilimia miamoja nadhani ni wakati wake sasa kujumuishwa kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal ili kutupa radha.
3) Damian Martinez mahala pa Woijcech Szczesny
Haya ni mabadiliko ya lazima kufanyika kutokana na kadi anayoitumikia Szczesny. Inasikitisha kuona mtu ambaye angeweza kuwa mbadala sahihi katika nafasi hii David Ospina ameumia hivyo kuikosa nafasi hii adhimu ya pengine kumshawishi Wenger kumpatia nafasi ya kwanza na hivyo kumwacha Martinez akikaa langoni.
4) Aaron Ramsey badala ya Alex Oxlade-Chamberlain
Chamberlain alitunukiwa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Hull, lakini kiwango duni alichokionesha kimenifanya kumtamani Ramsey akija na kushika pahala pa Alex, Natamani kumuona Santi Cazorla akiwa katika winga moja wapo ili kumpa
Aaron Ramsey acheze kama kiungo wa katikati ili aambatane na Jack Wilshere kwenye mfumo wa 4-1-4-1.
5) Laurent Koscielny mahala pa Per Mertesacker
Kama sijakosea Koscielny anatarajiwa kuwa fiti kwaajili ya mchezo huo na hivyo nadhani anastahili kuanzishwa sambamba na Chambers. Mertesacker hajaonesha uwezo wa juu sana msimu huu na mashabiki wengi wa the Gunners
kutokana na sare dhidi ya Hull siku ya jumaapili. Kumuacha Mertesacker nje ya kikosi kutamfanya arejee katika fomu yake ya kawaida.
Huo ni mtazamo wangu mimi sijaujua wakwako wewe. Fanya kama unauweka live hivi halafu tuone.
Post a Comment