0
Jose Mourinho amewahi kusema kuwa ukimuona meneja wa timu flani anamsukuama meneja wa timu nyingine tena katikati ya mchezo kama alivyofanya Arsene Wenger siku ambayo timu yake ilikua ikicheza dhidi ya Chelseal basi ujue amefanywa vibaya na tayari akili yake haiko kawaida.

Maneno hayo ya msema hovyo Jose Mourinho yanaonekana kuwa na ukweli ndani yake kwani kinachoonekana kwa Wenger kwa sasa ni kushindwa kabisa kukipanga kikosi chake licha ya kuwa angalau msimu huu amekua na kikosi kipana kiasi chake pamoja na  kuwa na tatizo la majeruhi wengi kikosini mwake, lakini kubwa zaidi akionekana kushindwa pia kutimiza ahadi zake za usajili azitoazo hadharani,

Alex Oxlade-Chamberlain wheels away after equalising for Arsenal against SpursĀ 

Kabla ya mchezo wa Hull Citty, Wenger alisema atahakikisha anamleta kiungo wa hadhi ya juu kwenye dirisha la usajili la mwezi January. Ikumbukwe huu ni mwezi wa kumi sasa na klabu ya Arsenal imeanza msimu kwa kumtumia Nacho Monreal kama mlinzi wa kati kutokana na tatizo la maumivu ya baadhi ya wachezaji wakongwe.

Monreal kweli ni mlinzi mzuri na ameisaidia sana Arsenal kutokana na umahiri wake lakini chini ya utawala wa Wenger mara kadha wa kadha tumemshuhudia akitumika kama kiungo hali amabyo itamlazimu kukubaliana nayo kwa takribani miezi mitatu ijayo kbla ya Wenger kutimiza adhima yake ya kumnunua kiungo wa hadhi ya juu Duniani. 

 Arsenal's Welsh midfielder Aaron Ramsey is substituted after being injured during the  Premier League derby

Kabla ya dirisaha la usajiri la majira haya ya joto kufungwa Arsenal ilikua ikiwazungumzia na kuwafuatilia wachezaji kadhaa akiwemo kiungo mkabaji wa klabu ya Sporting Lisbon William Carvalho lakini kilichokuja kuwaacha wazi midomo wadadisi wengi wa masuala ya soka ni kitendo cha Wenger kwenda kuchezesha mchezo wa hisani nchini Italy badala ya kupambana na kufanya usajili wa kukiimarisha kikosi chake katika siku hiyo ya mwisho ya dirisha la usajiri.

Katika hatua hiyo Arsenal ikajikuta angalau ikijipoza machungu kwa kumnasa Danny Walbeck kutoka kwa mashetani wekundu wa jiji la Manchester kalbu ya Manchester United.

 Danny Welbeck looks on during the North London derby against Tottenham Hotspur on Saturday

Lakini pia Wenger ameshindwa kumshawishi na kumrudisha nahodha wake wa zamani Cesc Fabregas, ambaye kwa sasa ameendelea kuthibitisha kuwa yeye ni kiungo bora kabisa na kutokana na ubora alionao amemfanya Diego Costa kung'ara na kuiwezesha kalabu yake ya Chelsea kukaa kileleni kwa tofauti ya pointi 5.

Kwenye majira ya kiangazi yaliyopita ilishuhudiwa Flamini akitua jijini London kwa madhumuni ya kufanya mazoezi na klabu ya Arsenal, na hatimaye kwenye mazoezi hayo kumshawishi mzee Wenger kuwa ni kiungo wa hadhi ya klabu ya Arsenal licha ya kuwa kwa wakati huo alikua ameachwa huru na klabu yake ya AC Milan kutokana na kuporomoka kiwango lakini pia kutaka kandarasi ya muda mrefu na Milan na hivyo kupewa kandarasi ya kuwatumikia washika mitutu hao wa jiji la London.

 Arsenal's Alex Oxlade-Chamberlain slots home the equaliser against local rivals Tottenham on Saturday

Kwenye msimu wake wa mwanzo alionekana kuwa msaada mkubwa sana kwa Arsenal huku mfumo wake wa kutumia mabavu na vurugu nyingi awapo uwanjani ukionekana kama ni suluhisho la matatizo ya kiungo waliyonayo Arsenal.

Mfumo wake huo wa kutumia nguvu nyingi unaonekana kutokuwa na maana tena kwani kama ulimwangalia kwa umakini Flamini kwenye mchezo dhidi ya Hull City unaweza ukawa shahidi jinsi ambavyo Mohamed Diame ilivyompeleka puta na kumfanya kuonekana lulu kwenye mchezo huo aliofanikisha kuisambaratisha safu ya kiungo ya Arsenal iliyolazimisha sare ya jumla ya magoli 2:2.

Flamini anaonekana kutumia nguvu nyingi sana kuliko hata walivyokua wakitumia akiana Roy Keane, Patrick Vieira au anavyotumia Daniele De Rossi katika kutekeleza majukumu yao ya kuziunganisha timu zao kwa nyakati tofauti.
Pamoja na Flamini lakini Jack Wilshere naye ameendelea kutufanya tuendelee kumuona Paul Scholes kama ni moja kati ya viungo tunaoweza kuwaita hakunaga kutokana na uwezo wake aliowahi kuuonesha wakati wa kipindi chake cha uchezaji.

Anapokea vizuri mipira, anakaba na kunyang'anya vizuri kabisa lakini tatizo lake linabakia kwenye suala la utoaji wa pasi na hasa za mwisho ambazo zinaweza kuzaa magoli.Wilshere hapigi pasi za uhakika kwani mpaka sasa akiwa kama kiungo mimi ninaona kuwa ajaitekeleza kazi yake hiyo ipasavyo hivyo kuifanya Arsenal pia kushindwa kucheza vizuri.

 Mikel Arteta sits and angrily throws his boot to the ground after injury forced him out of the Tottenham game

Hivyo ukiyaangalia matatizo haya ya kiungo kwa umakini utakuja kugundua kuwa endapo Wenger angefaya manunuzi ya viungo bora kabisa duniani au angeamua kumchezesha Ozil katika nafasi yake ya asili basi angalau Arsenal hii leo ingeendelea kuwapa furaha mashabiki wake.

Lakini kwa mfumo wa Wenger wa kuwa na maneno mengi kuliko utekelezaji ataendelea kuwafanya mashabiki wa Arsenal kuwa wanyonge duniani kutokana na matokeo mabovu na yasiyo tabirika ya klabu yao waipendayo. Halikadharika kitendo cha kutowatumia wachezaji kama Ozil na Carzola ipasavyo kwa kuwachezesha katika nafasi zao za asili inawafanya pia mashabiki hawa kuendelea kutabika kwa kutokuwa na uhakika na matokeo ya timu yao pindi iingiapo dimbani.


Arsene Wenger's side salvaged a point thanks to Oxlade-Chamberlain's first Gunners goal since February

Ni Wenger pekee anayeweza kuyatatua matatizo haya na hivyo kurejesha furaha kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal ulimwenguni.

Post a Comment

 
Top