Kocha wa klabu ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger hii leo ametoa taarifa nzuri na tamu masikioni mwa mashabiki wa klabu ya Arsenal mara baada ya kutangaza kuwa mshambuliaji wake raia wa ufaransa Olivier Giroud huenda akarejea uwanjani mapema kuliko ilivyokua ikidhaniwa hapo awali.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekua nje ya uwanja tangu mwezi wa August kutokana na maumivu ya kuvunjika mfupa wa mguu na sasa inatarajiwa kuwa huenda atarejea uwanjani mapema zaidi kuliko ilivyodhaniwa kutokana na matibabu yake kuendelea vizuri.
Hapo awali taarifa za kitabibu zilikua zikidai kuwa huenda mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa angekaa nje kwa takribani miezi minne hali ambayo kocha wake Arsene Wenger amesema kwa sasa inatarajiwa kuwa tofauti na mshambuliaji huyo atarejea mapema zaidi.
Mshambuliaji mpya wa klabu ya Arsenal aliyenunuliwa akitokea klabu ya Manchester United Danny Welbeck amekua akiiongoza klabu ya Arsenal katika sehemu ya ushambuliaji ya kalbu hiyo tangu kuumia kwa Giroud hivyo kurejea kwake mapema kutakuja kuongeza nguvu na ushindani katika klabu hiyo.
Post a Comment