Katika kile kinachoonekana dhahiri shahiri kuamua kutafuta njia ya mumfunga mdomo na kumrejesha nyuma katika mapambano yake dhidi ya uongozi wa kinabii wa TFF leo hii kamati ya nidhamu ya TFF imetoa tamko rasimi la taarifa ya kumfungia wakili Damasi Ndumbaro kutojihusisha na masuala ya soka kwa takribani miaka saba pasi na sababu za msingi kutajwa.
Katika taarifa hiyo iliyotolewa leo kwa waandishi wa habari kamati hiyo imesema kuwa imemfungia wakili huyo aliyejizolea umaarufu siku za hivi karibuni kwa umahiri waka katika kuwatetea wateja wake kwa kipindi cha miaka saba na kutakiwa kulipa faini ya pesa taslimu.
katika taarifa hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari kamati hiyo imedai kuwa Ndumbaro alikimbilia katika vyombo vya habari na kusema wazi kuwa, klabu
zimemuagiza kuwaambia TFF kuwa havipo tayari na havitakubali jambo hilo
litokee, huku akijiamini na kuchambua baadhi ya vipengele na mambo ya
sheria, Ndumbaro alivuka mipaka pale aliposema kuwa wanatafuta wastani
wa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na kupiga kura ya kutokuwa na imani na
rais wa Shirikisho, Jamal Malinzi.
Kikao cha juzi cha kamati ya nidhamu kimefikia uamuzi wa kumfungia, Ndumbaro na kumlilipisha faini kwa sababu.
1.Ndumbaro ambaye alizungumza
kama wakili wa klabu za ligi kuu kupitia, Bodi ya Ligi amekanwa ‘
hadharani’ na vilabu huku vikisema kuwa ‘ havikumtuma’ kuzungumza yale
ambayo alisema mbele ya vyombo vya habari.
2.Klabu zimesema alizungumza
kwa ‘ utashi’ wake mwenyewe, na si wao walimtuma.
‘ Kilichomuhukumu ni yeye kutaka kubadilisha maamuzi ya kamati ya utendaji ya TFF bila kuthibitishwa na wajumbe wa Bodi ya Ligi na kukubaliana. Kupingana maamuzi ya kamati ya utendaji ni kosa la kinidhamu. Ndumbaro amehukumiwa kutokana na makosa hayo na kama angezungumza kwa niaba ya klabu basi adhabu hiyo ingekwenda kwa kwao, lakini yeye alijizungumzia tu kama vile alivyotaka iwe.
Ukiangalia katika taarifa hiyo unaweza ukaona jinsi ambavyo njia ya kuzibana midomo inavyotafutwa kwa watu mbalimbali kwani kwa akili ya kawaida aliyoyasema Ndumbaro ni masuala ya kawaida na yenye ukweli mtupu kwani haihitaji hata darasa moja mtu kujua kuwa tangu TFF iingie madarakani haijaitisha mkutano mkuu jamboa ambalo ni lakikatiba na hivyo si haki kwa aliyeyasema hayo kufungiwa kwa sababu ya kusema ukweli.
Kama Ndumbaro amekurupuka na kujisemea ya kwake sasa iweje TFF hawakumkana Mbele ya Naibu Waziri mwenye dhamana ya habari tamaduni vijana na michezo Alhaji Juma Nkamia kuwa hakuwa mjumbe halali wa kikao kile kilichoitishwa naye katika hatua ya kutatua mgogoro uliokuwa unafukuta kwa wakati ule.
Lakini wakati Watanzania tulio wengi tukiwa na hamu kubwa ya kutaka kujua lini na wapi TFF itakutana na wadau wake na kujadili juu ya suala hilo halijapatiwa majibu leo TFF inaibuka na mapya ya kutangaza kumfungia mwakilishai anayesimama kwa niaba ya vilabu kwa minajiri ya kutetea maslahi yao.
Ninachokiamini mimi Ndumbaro si mwendawazimu wa kujiviaka joho la kuvisemea vilabu pasi na kuagizwa hivyo ninaimani kuwa adhabu iliyotolewa na TFF ipo katika misingi ya chuki, uhasama, kukomeshana na kuzibana midomo katika kuhakikisha kuwa madudu yanayofanywa na viongozi wakuu wa TFF hayaanikwi hadharani na wapenda maendeleo ya soka.
Ukiangalia suala lililopo mezani na hukumu iliyotolewa ni sawa na ile vijana wa kiswahili wanayoita kuuwa Mende kwa Nyundo kwani nakumbuka siku kadhaa zilizopita kulikua na sakata kati ya shirikisho la soka Duaniani FIFA na Franz Anton Beckenbauer mara baada ya Mjerumani huyo kushindwa kutoa ushirikiano kwa kamati maalumu ya shirikisho hilo iliyokua ikichunguza suala la Qatar kushinda nafasi ya kuandaa kombe la Dunia na adhabu yake ilikua ni kufungiwa kutojihusisha na masuala ya soka kwa takribani miezi mitatu (Siku 90), sasa haya ya Ndumbaro yanaibua maswali mapya kuwa je hii ni adhabu ya kikanuni au ya chuki.
Jana nikiwa kwenye kipindi cha Michezo Wiki hii ya Redio Jogoo 93.0 Mhz (Mshirika wa kuaminika mkoani Ruvuma) niliwaambia wenzangu niliokuwa nao kwenye kipindi ( Tamimu Adamu & Onesmo Emeran) kuwa kilichopo mbele ya kamati ya Nidhamu ya TFF ni kutaka kutafutiana sababu na kufungiana kwa muda mrefu kwenye lengo la kutaka kuzima mianya yote na viashiria vyote vya kuyafichua maovu yao ya kiutendaji yanayoendelea ndani ya TFF.
TFF MMEVUKWA NA NGUO CHUTAMENI MSITIRIKE UBABE HAUTAWASAIDIA KAMWE.
Hossam Hassan Ulaya. hossamulaya@gmail.com.
0755231571/0713281932
Post a Comment